Severo wa Napoli

Sanamu ya Mt. Severo ikitembezwa nyuma ya ile ya Mt. Severino.

Severo wa Napoli (alifariki Napoli, Italia, 29 Aprili 409) alikuwa askofu wa 10 wa mji huo kuanzia Februari 363.

Anasifiwa kwa juhudi zake za kutetea imani sahihi dhidi ya Waario pamoja na rafiki yake Ambrosi wa Milano aliyemuandikia barua[1]. Alipendwa naye kama ndugu, na kupendwa na waumini wake kama baba.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Aprili[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91851
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne